Thursday 27 July 2017

Coutinho aomba kwenda Barcelona

Bado dirisha la usajili linaendelea kushika kasika kasi na taarifa za chini chini zinadai kiungo wa Liverpool Phellipe Coutinho amemuomba kocha wake Jurgen Klopp amruhusu kwenda Barcelona.
Inafahamika kwamba Barca wanaihitaji sahihi ya Coutinho na wameshatuma ofa kwa Liverpool na wameshafanya mazungumzo na Coutinho ambaye yuko tayari kujiunga nao wakati wowote.
Taarifa nyingine za usajili ni kwamba baada ya habari kuzagaa kwamba Mbappe anakwenda Real Madrid sasa Pep Gurdiola maeingia katika mapambano na anataka kutoa kitita kikubwa zaidi kwa Monaco ili kumnasa Mbappe.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kwa sasa Harry Kane ndiye striker anayemkubali sana nje ya Chelsea lakini hawezi kumnunua kwani ana uhakika bei yake kwa sasa itakuwa iko juu sana.
Kiungo Jack Wilshaire hataki kuondoka nje ya jiji la London na anaona kama Arsenal wataamua kumuuza ni bora wamuuze humo humo London huku West Ham ikitajwa kama sehemu ambayo anaelekea Wilshaire.
Makamu wa raisi wa Monaco Vadim Vasylev amezikatisha tamaa klabu zinazowataka Fabinho na Lemar kwa kusema kwamba wachezaji hao ni muhimu na ana uhakika watabaki.

No comments:

Post a Comment