Monday 24 July 2017

Manchester United yaichapa Real Madrid

Timu hizi zitakutana katika mchezo wa super cup Agosti 8
Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1.
Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza.
Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari.
Haukuwa usiku mzuri kwa Lindelof ambaye aliendeleza makosa yake na kukosa mkwaju wa penalti.

United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika fainali siku ya Jumatano.

No comments:

Post a Comment