Thursday 20 July 2017

Lowassa kurudi tena kwa DCI baada ya wiki tatu

 Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Edward Lowassa leo July 20, 2017 ameripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuhojiwa ‘DCI’ kuhojiwa kwa mara ya nne.
Lowassa ametakiwa kurudi tena kwa DCI baada ya wiki tatu kutokana na kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa  Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani  akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

No comments:

Post a Comment