Friday 21 July 2017

Mbadala wa Msuva huyu hapa


Winga wa kimataifa wa Burundi, Baruan Yahya
Mchezaji huyo raia wa Burundi amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa wachezaji waliyo sajiliwa na Yanga SC.
“Nafurahishwa na uwezo wa wachezaji, Thaban Kamusoko na Ibrahim Ajib wanavipaji vya hali ya juu na uwezo wao unanipa kiu ya kufanya makubwa msimu ujao”.Amesema Baruan Yahya.
Mpaka sasa kikosi hicho cha Mzambia, George Lwandamina kina jumla ya wachezaji watano, kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

No comments:

Post a Comment