Monday 24 July 2017

Taarifa ya Ufafanuzi Toka Wizara ya Mambo ya Nje Juu ya Uhusiano wa Kibiashara na Serikali ya Kenya

Pix 01
Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Pix 03
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Pix 02
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo na kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Peter Sang.
Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

No comments:

Post a Comment