Thursday 20 July 2017

RC Gambo amewataka wananchi wa Arumeru kutovamia mashamba ya wawekezaji

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wakazi wa kijiji cha Maloloni Wilayani Arumeru kuacha kuvamia mashamba ya wawekezaji pindi inapotokea migogoro ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo umwagaji damu na uharibifu wa mali.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Bw. Gambo amesema ni vyema migogoro hiyo inapojitokeza ikatatulia kwa njia ya mashauriano kwa pande zinazo kinzana badala ya wananchi kujichukulia sheria mikononi ya kuvamia mashamba hayo.
"Ni kosa kwa wananchi kuvamia mashamba ambayo yana hati miliki halali, serikali ya haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea tutachukua hatua kwa wale wote watakaobainika kufanya uvamizi huo", amesema Gambo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya Meru, Christpher Kazeri amesema wamekua wakiifanyia kazi migogoro hiyo huku afisa mipango miji wa Halmashauri hiyo Shahidi Chuma, ameahidi kutafuta suluhu ya migogoro hiyo baina ya kijiji cha Magadini na maloloni.

No comments:

Post a Comment