Sunday 30 July 2017

Tetemeko dogo la ardhi latokea Karagwe

  Image result for Kagera
Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika  Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa  kutokea.
Ofisa wa Wakala wa  Jiolojia Tanzania, Gabriel Mbogani amesema ili kupata uhakika wa tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa wapo makini  baada ya kupatiwa semina kutokana na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa  na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko  wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo  kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea  kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda  gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye kuwa kubwa.


Mkazi wa mji mdogo wa Kayanga, Elieth Kikaka  amesema alitoka nje ya nyumba baada ya tetemeko hilo kwa kuwa yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani Kagera hivyo linapotokea ni lazima  kuchukua tahadhari.

No comments:

Post a Comment