Thursday 27 July 2017

Vyuo Vikuu Nje ya nchi katika maonesho ya TCU Dar es salaam, Kutana na timu nzima ya Global Education Link kwa udahili wa papo papo.

GLO1
Mkurungezi mtendaji Mkuu  wa (GEL) Abdulmalick Mollel akimuelezea Huduma za Taasisi hiyo  Dr.Charles Msonde ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa Mitihani( NECTA) wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na (TCU) Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
GLO2
Mfanyakazi wa Taasisi ya  Global Education Link Bw. Liberius John akiwa anatoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda hilo ili kujionea huduma zinazotolewa na (GEL)
GLO3
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliotembelea maonyesho hayo wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la Global Education Link.
GLO4
Wafanyakazi Mbalimbali wa Taasisi ya Global Education Link wakiwa kwenye banda hilo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
Global Education Link (GEL) ambao ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa kwa wanafunzi wanaotaka  kufanyiwaudahili  ili kujiunga na vyuo vikuu vya nje  wanaweza kufika katika banda la na kupata maelezo hukusu vyuo hivyo katika maonesho ya TCU jijini Dar es salaam ,wanafunzi,wazazi na walezi mnakaribishwa ili kupewa miongozo ya udahili wa vyuo vikuu nje ya nchi,katika ngazi ya diploma mpaka shahada ya udhamili.
Akizungumza Mkurungezi wa Global Education Link(GEL),Abdulmalik Mollel amesema katika dhima ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda inahitajika rasilimali watu wa kutosha ili kukidhi mahitaji hayo
 
Mollel amesema wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi wajitokeze katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kukutana na timu nzima ya Global Education Link kwa ushauri na utaratibu wa udahili wa papo kwa papo.

No comments:

Post a Comment