Wednesday, 24 August 2016

Mbowe kunyang’anywa Bilicanas mwezi huu

  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amesema mmiliki wa jengo la Club ya Bilicanas, Freeman Mbowe ni miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo waliopewa notisi inayoishia mwezi huu.

Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam, Mchechu amesema Mbowe anadaiwa malimbikizo ya kodi.

Hata hivyo amesema suala hilo halina uhusiano na siasa za Ukuta kwani mbali na Mbowe zipo taasisi na watu binafsi wanaodaiwa.

“ Zipo pia taasisi za serikali zikiwemo wizara na idara ambazo mwezi zitatimuliwa kwenye majengo wanayotumia.”

No comments:

Post a Comment