Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi, Dhahir Athuman Kidavashali amesema polisi walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa kuna kundi la majambazi wanataka kuvamia nyuimbani kwa mfanyabishara Gadi Mwainunu na ndipo wakaweka mtego nyumbani kwa mfanyabishara huyo na ndipo watu hao wakitumia usafiri wa pikipiki mbili wakafika eneo hilo na kukabiliana na askari.
Kamanda Kidavashali amesema kuwa baada ya kuuawa watu hao walipekuliwa na kukutwa na bunduki mbili pamoja na silaha nyingine za jadi.
Miili ya watu hao ambao bado hawajatambuliwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe Makandana, ambapo kamanda Kidavashali ametoa wito kwa ndugu na jamma kwenda kuwatambua, huku akitoa wito maalum kwa watu wanaojihusisha na uhalifu.
Hilo ni tukio la pili la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuuawa kwenye majibizano ya risasi mkoani Mbeya, ambapo mwezi Aprili pia polisi mkoani Mbeya waliwaua majambazi watatu wilayani Chunya.
No comments:
Post a Comment