Saturday 16 July 2016

Victoria Azarenka afichua ni mjamzito

 Azarenka
Mshindi mara mbili wa mashindano ya Australian Open Victoria Azarenka has amefichua kwamba ana mimba.
Rais huyo wa Belarus mwenye umri wa miaka 26 amesema anapanga kurejea katika uchezaji baada ya kujifungua mwishoni mwa mwaka huu.
Azarenka na mpenzi wake waligundua kwamba alikuwa mjamzito alipokuwa anauguza jeraha lla goti.
"Tuna furaha sana na najihisi kubarikiwa kwamba nitaanza safari hii ya kusisimua,” amesema Azarenka, ambaye ameorodheshwa nambari sita kwa ubora duniani.
"Nimetiwa moyo sana na wanamichezo wengine wa kike ambao huweza kurejea kushindana baada ya kujifungua na ninapanga kufanya vivyo hivyo.”

 
Azarenka alishinda Australian Open mwaka 2012 na 2013, miaka ambayo pia alifika fainali US Open lakini akashindwa.
Hajacheza tangu aondoke uwanjani raundi ya kwanza mechi ya French Open dhidi ya Mwitaliano Karin Knapp mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment