Sasa mbaya zaid ni kitendo cha mwenyekiti wa soko kuwachangisha wafanya biashara wa sehemu fulani ndani ya soko hilo sh.2000/= kwa kichwa kwa siku kama mradi wake binafsi wa siri akidai ni lazima watoe ili waendelee kufanya biashara,vinginevyo wapishe ukarabati had uishe kitu ambacho ni kibaya, ukarabati unaonyesha hauishi leo wala kesho au umesimama kabisa,
Kwa sasa kwa siku unatozwa sh.2000/=ya muheshimiwa,sh.500/= ya kila kizimba,sh.300/= ya ushuru wa siku, Inamaana usipo lipa sh.2000/= unafukuzwa ukakae ktk eneo lisilofikiwa kwa urahisi na wateja wa biashara husika.
Je,hii ndio kasi ya maendeleo kwa wote?,au kwa mtu binafsi?, na sasa kesha fanikiwa kununua na gari ya kutembelea, hatuyajui maendeleo yake binafsi yaliyofichika, Ukweli ni kwamba kawakusanya wafanya biashara pamoja (upande)ili kwa anaetaka nafasi sehemu nzuri ya wazi akubali kutoa sh.2000/= kila siku.
Picha za sehemu inayo karabatiwa hapo sokoni..
No comments:
Post a Comment