Friday 15 July 2016

usiyoyajua kuhusu ligi ya China

Amezitosa timu za Chelsea pamoja na Everton za Uingereza, ameingia kwenye rekodi ya kundi la wachezaji kumi wa juu wanaolipwa zaidi duniani. Atalipwa kiasi cha Euro milioni 13 pesa ambazo Graziano Pelle amemshusha Wayne Rooney kwenye orodha ya wanaolipwa pesa nyingi hadi nafasi ya sita.
Pelle ambaye mshahara wake kwenye klabu ya Southampton ulikuwa ni Euro milioni 2.2 kwa mwaka amepanda chati ghafla hivyo baada ya kusajiliwa na klabu moja ya China, kule walipo kina Demba Ba, Hulk, Scolari  tayari kwa kusakata kabumbu.

Yawezekana unajiuliza maswali mengi kuhusu ligi hii ya china, makala hii inakupa mambo saba (7) muhimu kuhusu ligi ya soka nchini humo

Ligi ya china ina miaka 12 tangu kuanzishwa
Ping An Chinese Super league ilianza mwaka 2004 baada ya kubadilishwa jina iliyokuwa ligi daraja la kwanza Jia –A league ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1994 na kuongezeka kwa timu kutoka kumi na mbili hadi kumi na sita. Ping An ni kampuni ya bima iliyopewa haki ya kumiliki jina la ligi tangu mwaka 2014. Udhamini wao una thamani ya Yuan milioni 150 kwa mwaka.

Msimu mpya unaanza wakati ligi za Ulaya zinaisha
Wakati mwezi Febuary hadi March ni kipindi ambacho ligi za Ulaya zinaelekea ukingoni, kwa upande wa China ndio mwanzo wa msimu mpya. Kipindi hicho kwa upande wa China ndio ambacho nchi ipo kwenye majira ya kiangazi, Ligi inamalizika November au December.

Bingwa pamoja na washindi wengine wawili wanawakilisha nchini kwenye klabu bingwa barani Asia, pia timu mbili zinashuka daraja na mbili kupanda.

Kashfa za kupanga matokeo

Mwaka 1998 iliyokuwa ligi daraja la kwanza iliwahi kupatwa na tuhuma za kupanga matokeo hivyo kupunguza mvuto wa ligi kwa wapenzi kutokwenda viwanjani kutazama mechi za Ligi. Mwaka 2010 Serikali iliingilia kati na kuwakuta na hatia ya makosa ya rushwa waliokuwa  makamu wa Rais wa chama cha Soka (CFA), Xie Yalong, Nan Yong na Yang Yimin na kuadhibiwa.

2011 mastaa waanza kuja baada ya rushwa
Vilabu vya Guangzhou Evergrande na Shanghai Shenhua ndivyo vya kwanza kuanza uwekezaji wa wachezaji wa kigeni baada ya chama cha soka cha China (CFA) kusafishwa kwa makosa ya rushwa. Miongoni mwa wachezaji wa mwanzo ni Didier Drogba, Seydou Keita na Nicolas Anelka.

Pia ulikuwa mwanzo wa makocha wakubwa kama Marcelo Lippi kocha alieipa Italy kombe la dunia mwaka 2006.


Wachezaji wa kigeni watano kwa timu
Kwa mujibu wa sera ya ligi yao, kila timu inaweza kusajili idadi ya wachezaji wakigeni wasiozidi watano pia idadi ya juu ambayo timu itawatumia wachezaji hao kwenye mchezo mmoja ni wachezaji wanne.

Misimu 12 mabingwa saba
Tangu msimu wa kwanza mwaka 2004 ulipoanza ubingwa wa Ping An Chinese League umechukukuliwa na timu saba tofauti, huku Guangzhou Evergrande wakitwaa mara tano mfululizo tangu mwaka 2011. Pia timu ya Shandong Luneng imetwaa mara tatu (2006, 2008 na 2010). Timu za Beijing Guoan, Changchun Yatai, Dalian Shinde na Shenzen wakitwaa mara mojamoja

Wabrazil wanatisha kwa ufungaji bora
Wakati Wakiamini wamepungukiwa na wapasia nyavu, huko china wao ndio vinara wa kupachika mabao. Tangu mwaka 2013 wao ndio wameshinda tuzo ya ufungaji bora. Tangu mwaka 2004 wabrazil wametwaa kiatu cha ufungaji bora mara tano.

No comments:

Post a Comment