Tuesday 19 July 2016

Shule 70 za upili zateketezwa Kenya

 
Shule 70 za upili zimeteketezwa moto na wanafunzi wenye hasira nchini Kenya.
Waziri wa elimu nchini humo Fred Matiangi ameiambia kamati ya bunge iliyoundwa kupeleleza wimbi la shule kuteketezwa kuwa hakujakuwa na hata wanafunzi 20 waliohukumiwa kwa kuteketeza mali ya umma kwa sababi moja au nyingine kati ya visa 317 zilizoripotiwa kati ya mwaka wa 2007 -2016.
  8
Shule 317 ziliteketezwa kati ya mwaka wa 2007 -2016.
''Endapo serikali itachukua hatua dhidi ya wale watakaoteketeza mabweni yao au hata madarasa bila shaka wale wanaoiga wataogopa'' alisema bwana Matiangi.
''Mara nyingi tumegundua kuwa zile shule ambazo zinachunguzwa kwa sababu ya wizi wa pesa za kufadhili masomo ya bure na fedha za kununua vitabu vya wanafunzi zinateketezwa kwa sababu finyu sana''.

 
 
Walimu 15 wakuu wanachunguzwa kulingana na taasisi inayosimamia walimu nchini Kenya TSC.
Walimu 15 wakuu wanachunguzwa kulingana na taasisi inayosimamia walimu nchini Kenya TSC.
Wandani wa maswala ya elimu nchini Kenya akiwemo katibu mkuu wa muungano wa walimu KNUT bwana Wilson Sosion amelaumu mabadiliko ya sera yaliyotolewa na wizara ya elimu kama vile kuongeza muda wa muhula wa pili, na kupiga marufuku likizo ya kati ya muhula ujao mbali na kupiga marufuku wazazi kuwatembelea wanafunzi shuleni kama sababu zinazochochea wimbi hili la moto shuleni.
 
Katibu mkuu wa muungano wa walimu KNUT bwana Wilson Sosion amelaumu mabadiliko ya sera yaliyotolewa na wizara ya elimu kwa machafuko haya yanayoshuhudiwa
Hata hivyo waziri Matiang'i akijitetea aliiambia kamati hiyo ya bunge kuwa kabla ya mabadiliko hayo kutangazwa shule 90 zilikuwa zimeteketezwa tayari.

No comments:

Post a Comment