Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo anatarajiwa kuanza kucheza michuano ya Europa League, wakati timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji itakapoikaribisha FK Buducnost Podgorica ya Montenegro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Samatta anatarajiwa kupangwa leo kwa sababu amefanya vizuri katika michezo ya kujipima nguvu kujiandaa na mashindano hayo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu Ulaya, akifunga mabao matatu katika mechi nne.
Timu hizo zitarudiana wiki moja baadaye, yaani Julai 21, mwaka huu Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica nchini Montenegro na mshindi wa jumla atasonga mbele.
No comments:
Post a Comment