Wednesday 13 July 2016
Rais Barack Obama wa amewahimiza Wamarekani kutovunjika moyo
Rais Barack Obama wa amewahimiza Wamarekani kutovunjika moyo kutokana na visa vya ubaguzi wa rangi na leo ni siku ya mwisho kwa David Cameron kuhudumu kama waziri mkuu Marekani.
Rais Barack Obama amewaomba raia Marekani wasivunjike moyo kuhusu wasiwasi wa ubaguzi wa rangi akieleza kuwa tiafa hilo halijagawanyika kama inavyodhaniwa.
Alikuwa akizungumza katika misa ya wafu ya maafisa wataano waliopigwa risasi na kuuawa na mwanajeshi wa zamani aliyetaka kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanaume weusi na polisi.
Bw Obama amesema polisi hawapaswi kuonekana kama walio na ubaguzi.
Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, limeishutumu serikali ya Misri kwa kuwapoteza watu kwa lazima ili kutishia na kuzima upinzani nchini. Amnesty linasema mamia ya wanafunzi wanaharakaati wa kisiasa na waandamanaji baadhi wakiwa na umri wa hata miaka 14 wamepotea
Leo ni siku ya mwisho kwa David Cameron kushikilia wadhifa wa waziri mkuu wa Uingereza baada ya kuhudumu kwa miaka 6.
Cameron alitangaza uamuzi wake kujiuzulu mwezi uliopita baada ya kushindwa katika kura ya maoni kuhusu uanachama katika Muungano wa Ulaya.
Anayemrithi ni Theresa May, aliyeidhinishwa kama kiongozi mpya wa chama cha Conservative Jumatatu.
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amezuru eneo kulikotokea ajali ya treni iliyosababisha vifo vya watu 23 kusini mwa Italia.
Ameahidi uchunguzi kamili utafanyika. Bado jitihada za uokoaji zinaendelea.
Brazil inasema inatoa dola milioni 24 za ziada kwa jeshi kushinikiza usalama kufuatia kuwadia mashindano ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro mwezi ujao. Zaidi ya maafisa 80,000 wa polisi na wanajeshi watapiga doria katika mitaa ya Rio wakati wa mashindano hayo.
Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, anasema wanadiplomasia wa nchi hiyo nchini Chile wangepaswa kusema kitu kuhusu ukiukaji wa haki za binaadamu katika eneo linalotawaliwa kisiri na jamii ya Wajerumani katika miaka ya 60 na 70. Eneo hilo liliundwa na aliyekuwa afisa wa Nazi.
Jumba la ukumbusho la mauaji ya kimbari ya wayahudi huko Washington limewataka wageni kutocheza mchezo maarufu wa simu "Pokemon Go" wakiwa katika jumba hilo, likieleza kwamba ni ukosefu mkubwa wa heshima.
Mchezo huo unaruhusu wachezaji kuwasaka na kuwakamata viumbe vya kidijitali katika maeneo ya kihalisia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment