Wednesday 13 July 2016

Mbunge wa EAC Hafsa Mossi auawa Burundi

 Mossi
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.

 
 
  Hafsa Mossi Facebook
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo#Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,” ameandika kwenye Twitter.

Bi Mossi alitetea sana haki za wanawake.

No comments:

Post a Comment