Wednesday 20 July 2016

Man United kujifua China

Kikosi cha Mashetani wekundu Manchester united kimeenda China katika kujiandaa na msimu mpya.Wakiwa huko China, United watacheza mechi mbili ya kwanza watacheza na klabu ya Borussia Dortmund mjini Shanghai, siku ya ijumaa na kisha jumatatu watacheza na Manchester Man City,jijini Beijing.
Jumla ya wachezaji 25 ndio wako kwenye msafara wa timu hiyo wakiwamo nyota wapya Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan pamoja na Chipukizi tisa toka chuo cha soka cha Man United, huku wachezaji wengine walioshiriki michuano ya ulaya wakiachwa kuendelea kupumzika.

Man United wanakwenda katika ziara hiyo wakiwa chini ya mkufunzi Jose Mourhino mwenye kibarua cha kurudisha thamani ya timu hiyo .

No comments:

Post a Comment