Mama Theresa May ameteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza leo
Mama Theresa May (59) wa chamacha Wahafidhina (Conservative Party) leo
ameteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wa pili mwanamke (baada
ya Margaret Thatcher aliyeongoza kati ya mwaka 1979 hadi 1990 na
Waziri mkuu wa 12 tokea utawala wa Malkia Elizabeth, na Waziri Mkuu wa
76 wa Uingereza) katika hafla ya faragha iliyofanyika katika kasri ya
Malkia Elizabeth jijini London. Na tayari Malkia amemwomba aunde
serikali, kuirithi ya Waziri Mkuu wa zamani David Cameron aliyeachia
ngazi baada ya kura ya maoni iliyowafanya Waingereza wajitoe Umoja wa
nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment