Waumini 30 wa dini ya kiislamu
wamekufa maji Kaskazini mwa Pakistan baada ya mafuriko ya ghafla kukumba
eneo hilo na kusomba msikiti wao .
Halmashauri ya kukabiliana na
majanga nchini humo inasema kuwa hakuna aliyesalia hai katika msikikiti
huo wa Ursoonulioko katika wilaya ya Chitral.Vyombo vya dola vya utabiri wa hali ya anga vinasema hii ndio mara ya kwanza kabisa kwa mafuriko makubwa na yenye kina kirefu zaidi kuwaikukumba eneo hilo la Kaskazini mwa Pakistan.
Eneo hilo lipo kimo cha takriban mita 8,000 juu ya usawa wa bahari.
Mafuriko katika eno hilo mwaka uliopita yalisababisha vifo vya watu kadha na kuharibu madaraja.
No comments:
Post a Comment