Sunday, 24 July 2016

Hata mumsajili Samatta hamtafanikiwa - Kiiza

Mshambuliaji aliyeachwa na wanamsimbazi 'Simba', Hamisi Kiiza amesema timu hiyo haiwezi kupata mafanikio hata kama itasajili wachezaji wote nyota wanaotamba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amekwenda mbali zaidi na kusema hata kama wakimsajili Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji haitakuwa na mafanikio hadi baadhi ya viongozi ambao hakutaka kuwataja waondoke madarakani.

Kiiza ametupiwa virago kwenye kikosi cha msimu ujao wa Ligi na uongozi wa timu hiyo, licha ya kushika nafasi ya pili kwa ufungaji bora kwa kufunga mabao 19, kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment