Balozi wa Kampeni ya Kili
Challenge Msanii Mrisho Mpoto amekonga nyoyo za mashabiki na wafanyakazi
wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwenye mnada maalumu wa bidhaa
mbalimbali za kuchangia fedha za Kampeni ya Kili Challenge kwenye ukumbi
wa Lapa Mchauru Mkoani Geita.
Kili Challenge ni mfuko
unaochangisha fedha kila mwaka kwa kudhamini watu kupanda mlima
Kilimanjaro ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana na janga la
ukimwi Tanzania. Mfuko huu unaratibiwa na Mgodi wa Geita (GGM) kwa
ushirikiano na Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (TACAIDS) pamoja
na wadau wengine mablimbali. Hadi sasa zaidi ya Taasisi
30zinazojihusisha na Ukimwi zimenufaika na mfuko huu wa Kili Challenge
na watu zaidi ya 500 kutoka duniani pote, wamepanda mlima Kilimanjaro
kupitia mfuko huu.
Akiimba kwa hisia Mrisho Mpoto
pamoja na Msanii mwenzake Mwimbaji wa mziki wa “Live” Ibrozama Mkungwe
maarufu kwa jina la “Beka” walitumbuiza wimbo wa “Sauti Nenda” remix
ikiwa ni mahususi kuwakumbusha watanzania kwamba Ukimwi bado upo na ni
jukumu la kila mmoja wetu kuchukua hatua dhaditi katika mapambano hayo.
Ukimwi.
Akizungumzia Kampeni ya Kili
Challenge, Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw
Terry Mulpeter alisema kuwa mwaka huu Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa
kushirikiana na tume ya kudhibiti na kupambana na UKIMWI(TACAIDS) na
wadau wengine wanatarajia watu zaidi ya 100 watashiriki katika kupanda
mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia baiskeli kwa jumla ya siku 7
ili kuchangisha fedha na kuisaidia serikali katika mapambano dhidi ya
Ukimwi.
Zoezi rasmi la kupanda Mlima
Kilimanjaro litaanza tarehe 16 Julai ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
No comments:
Post a Comment