Usiku wa siku kama ya leo (yaani Jumapili ya tarehe 3-7-2016) niliamka usiku kwa ajili ya daku, Ndipo nilipogundua jicho langu la kushoto halioni kabisa na jicho langu la kulia lina uoni wake ulikuwa mdogo.Ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu.
Najua madaktari mbali mbali wa hapa nchini walifanya kila jitihada za kunusuru macho yangu ila bado ufumbuzi wa tiba yangu bado haujapatikana. Ndio maana naenda kujaribu India.na Insha Allah Mungu atanivua mtihani huu.
Kiukweli hawa madaktari niwashukuru sana kwa jitihada zao.Rafiki yangu na kaka yangu Dkt. Mohammed wa wizara ya afya, Dkt. Mahunda wa Ocean Road, Dkt. Dalla, Dkt. Chibuga na Dkt. Hassan wa CCBRT na pia Dkt. Datoo wa clinic ya pale Shoppers Plaza Miikocheni. Vile vile Madaktari wa Kituruki pale katika hospitali yao ya International eye clinic maeneo ya Moroco pamoja na wauguzi wao.Mungu atawalipa Insha Allah.
Kipekee niwashukuru ndugu na rafiki zangu wa KT shop. Hapo mimi ndio
maskani yangu jioni.Hawa ni zaidi ya binadaam. Kisasa tungesema show
nzima ya safari wanasimamia wao.Wamefanya jitihada zote na kiukweli bila
wao sijui ingekuwaje.Kwa wiki zote mbili wamekimbizana na mimi ugonjwa
wangu bila kuchoka.
Pia niishukuru ofisi yangu klabu ya Simba kwa zaidi ya wema
walionifanyia.Niwashukuru viongozi wote, Friends of Simba.wanachama na
wapenzi wote wa Unyamani kwa kila jambo na dua zao
walizonifanyia..Kiukweli sijutii kupenda na kufanya kazi Simba.
Niishukuru pia serikali ya nchi hii. Nimepokea salaam kutoka kwa Waziri
wangu wa michezo.Mhe Nape. Salaam toka kwa waziri na naibu waziri wa
afya.Mh Ummy na Dkt. Kigwangallah. Nimepokea pia salam toka kwa rafiki
zangu manaibu waziri Mh Mavunde na Dkt. Possi.
Lakini kipekee kwa waziri wangu wa mambo ya ndani ya nchi. mtani wangu
Mh Mwigulu Nchemba ambae yeye mwenyew alikuja kuniona na kwa niaba ya
serikali ameahidi kunisaidia kwa kila hali niweze kupona.
Na kwa hapa nisiache kumshukru mwambata wetu wa afya katika ubalozi
wetu nchini India.Dkt. Goroka kwa kusaidia kupatikana kwa hospitali
India.Pia nimshukuru Profesa Mohamed Janabi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete ya hospitali Taifa Muhimbili kwa ushauri wake wa kitaalam
(nafurahi kusikia jana amethibitiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
hiyo nyeti, homgera sana Prof! Unastahili kabisa) .sambamba na daktari
wetu wa Simba.
Sitatenda haki kama sitawashukuru viongozi wakuu wa TFF Rais Jamal
Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa kwa kila jambo walilonifanyia.
Kipekee niwashukuru viongozi wa dini. mashekh na maustaadh kwa dua zao
kwangu.sambamba na wachungaji ambao walikuja hadi kwangu
kuniombea..Asanteni sana watu wa Mungu.
Nisisahau kuwashukuru watani zangu Yanga kwa mchango wao kwangu... Hususan mropokaji ๐๐ wao Jerry Muro.
Nita-mmiss sana kwa fujo na kebehi zake. Ninamuomba awaandikie TFF
kuomba radhi na kisha yeye naye ajirekibishe kidogo bana....Nna imani
TFF nao wanaweza kupitia kamati zao wanaweza kuangalia namna sahihi ya
kulimaliza hili kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini. Muhimu Jerry apime
tu kauli zake. Mpira si kashfa wala kebehi za kuudhi..na si uadui hata
kidogo.
Mwisho niwashukuru ndugu zangu wa Kariakoo Family Development Foundation
(KFDF) chini ya mwenyekiti wetu Mohamed Bhinda. Hawa ni Alfa na Omega
kwangu Kuanzia niliokuwa nao vjana wa Al-Ahly hadi KFDF. Pamoja nao watu
wangu wa nguvu.whatsapp groups zote ambazo zimeniombea sana na
kunifariji katiika kipindi hiki kigumu.sambamba na kuja kunijulia hali.
Nikiwasahau wanahabari nitakuwa wa ajabu..Wamefanya kazi kubwa ya
kuwahabarisha na kuwapa maendeleo yangu kila siku kupitia vyombo vyao.
Asanteni sana wote! My family. ndugu zangu. jamaa na marafiki
wote.nimejua kwa sasa Haji nna watu na nnamuomba mungu niendelee
hivihivi na tabia zangu njema nizilojaaliwa na Manani.Msiache kuniombea
kwa kila hatua.kuanzia safari yangu.matibabu na kuiombea familia yangu
inayobaki hapa nyumbani.
Nawapenda sana. Mungu awabariki sana.
Haji S.Manara
No comments:
Post a Comment