Gugu Zulu akiwa na mke wake
Kifo chake kimethibitishwa na taasisi ya Nelson Mandela iliyokuwa imeandaa upandaji huo wa mlima Kilimanjaro ujulikanao kwa jina la Trek4Mandela.
Zulu alikuwa sehemu ya kundi la waafrika Kusini wengine waliokuwa wakipanda mlima huo akiwemo mke wake, Letshego Zulu.
Picha ya mwisho aliyoweka kwenye Instagram ilikuwa jana Jumapili.
Jumamosi pia alipost nyingine inayomuonesha akiwa na mke wake na kuandika:
Made it though day2. My wife is doing fabulous, she has even learnt the local language. Am having flu like symptoms and struggling with the mountain but taking it step by step!! Today we managed to see our destination and our camp is literary above the clouds!! Bring day 3.”
Zulu alikuwa dereva wa mbio za magari mwenye mashabiki wengi na alikuwa akiendesha magari ya Volkswagen. Ameacha mke na mtoto wa kike mwenye mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment