Bw.Amil Shivji akitangazwa kuwa mshindi tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora Bw.Amil Shivji akipokea tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora
Usiku wa jana ulikuwa
ni wa furaha ya aina yake kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakiwania tuzo
kwenye tamasha la kimataifa la filamu la ZIFF lililofanyika Zanzibar na
miongoni mwa washindi hao ni Amil Shivji,ambaye pia ni mwalimu wa
masuala ya uandaaji filamu kwenye idara ya sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar
Es Salaam.
Bw.Amil kupitia filamu
ya AISHA iliyotengenezwa na kampuni ya Kijiweni Production kwa
ushirikiano na shirika la Uzima kwa Sanaa(UZIKWASA) lilipo Tanga,kwa
ujumla ilijishindia tuzo takriban nne katika kipengele
kilichoshindanisha filamu za kiswahili, maarufu kama “bongo movie”.
Filamu ya AISHA
iliyotengenezwa Pangani-Tanga, imekwishachezwa kwenye zaidi ya matamasha
thelathini(30) duniani, iliweza kuibuka kinara kwenye ZIFF kwa kutoa
muongozaji bora(Omar Chande), muigizaji bora wa kike(Godliver Gordian),
filamu bora(AISHA) na mhariri bora wa filamu(Momose Cheyo).
Mtengenezaji huyo wa
filamu aliyewahi kujinyakulia tuzo kadhaa kupitia filamu za SHOESHINE
pamoja na SAMAKI MCHANGANI, akitoa ushauri kwa vijana, wasanii chipukizi
na pia wasanii wakongwe aliwasihi wasidharau umuhimu wa kuingia
darasani kujinoa zaidi na kupata maarifa.
Bw.Amil aliongeza,”hata
kama chuo si chaguo la kwanza ama hauchukulii kwa uzito, kuna warsha
nyingi sana ambazo zinasaidia kukuza kipaji na uzoefu katika
utengenezaji wa filamu. Tafadhalini endeleni kusoma, kudadisi mambo
mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni, na daima ujiulize filamu zako
zitaongelea kuhusu nini”.
Akiwashukuru wadau wa
filamu alisiwasisitiza wajue tu kwamba Kijiweni productions ipo, na
itaendelea kupambana na mifumo inayokandamiza na kunyanyasa watanzania
na watu wote bila kujali rika, rangi au jinsia ya mtu.
Tamasha hilo la filamu
huandaliwa kila mwaka na kushirikisha maonesho ya filamu na sanaa
mbalimbali, utoaji tuzo na mafunzo kwa watengenezaji wa filamu
No comments:
Post a Comment