Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa
kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa
kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
Na Kalonga Kasati
Waziri wa afya maendeleo ya
Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto ameagiza watumishi wa nne wa MSD
waandikiwe barua ya kusimamishwa kazi kutokana na kukiuka taratibu za
manunuzi.
Watumishi hao ni Mkurugenzi wa
Kanda na huduma kwa wateja Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha na
Mipango Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja pamoja na
Mkurugenzi wa manunuzi Hery Mchunga.
Wakati huohuo watumishi wa Wizara
ya Afya , maendeleo ya Jamii , jinsia , Wazee na Watoto kitengo cha
Afya ya Uzazi na Mtoto tayari wametekeleza agjizo la Rais John Magufuli
la kuhama katika ofisi hizo ili jengo hilo litumike kwa ajili ya
wazazi.
Juzi Rais Magufuli aliagiza
watumishi wa wizara hiyo kitengo cha afya ya uzazi na mtoto kuhama
katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- ilitumie
kama wodi ya wazazi.
Zoezi la kuhama lilianza tangu jana na kuendendela leo asubuhi kwa ushirikiano kati ya Wizara ya afya na MNH .
Katika agizo hilo Mkurugenzi Mkuu
wa Bohari ya Dawa –MSD- Laurean Bwanakunu amekabidhi vitanda 120 ,
madogoro 120 , Vitanda vya kuzalishia 10, vitanda vya watoto njiti 10
pamoja na mashuka 480 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 88. 7.
Akipokea vifaa hivyo Waziri Ummy
amemshukuru Rais Magufuli kwa kuonesha kuguswa na changamoto
zinazoikabili sekta aya afya nchini na kuzitafutia ufumbuzi .
Pamoja na mambo mengine Waziri
Ummy ameagiza kupatiwa taarifa ya hali ya vitanda kila siku katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na hospitali nyingine za serikali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence Museru amemhakikishisa Rais
Magufuli kwamba hakuna mama mjamzito atakaye lala chini na kueleza kuwa
tatizo kubwa lilikua ni nafasi hivyo kutokana na agizo hilo wamepata
nafasi itakayochukua vitanda zaidi ya 120 .
Waziri Ummy Mwalimu Akipokea Msaada Wa Magodoro-Muhimbili
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kupokea msaada wa magodoro 120 kwa ajili ya wazazi
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Leo. Msaada huo umetolewa
na Bohari kuu ya Dawa nchini.
Kutoka Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dk UlisubisyaMpoki, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Bohari Kuu ya Dawa, Laurean Bwanakunu akitoa maelezo kabla ya kukabidhi
msaada wa magodoro kutoka katika bohari hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipokea msaada wa magodoro
kutoka Bohari Kuu ya Tanzania (MSD).
No comments:
Post a Comment