Mkuu wa
wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako alipofika ofisi
ya mkuu huyo wa wilaya na kuzungumza mambo machache na Wakaguzi wa
elimu na maofisa elimu wa wilaya ya Hai.
Waziri Ndalichako akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Hai,wakiwa katika kikao kidogo na Waziri Ndalichako.
Mkuu wa
wilaya ya Hai,Anthony Mtaka (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi ,Prof Joyce Ndalichako aliyefanya
kikao kidogo na watumishi wa Elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
Waziri Prof Ndalichako akizungumza na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akimsikiliza kwa makini Prof Ndalichako.
Waziri Prof Ndalichako akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kwa maofisa elimu na wakaguzi wa elimu katika wilaya ya Hai.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mabondia Said Mbelwa Na IbrahimuTamba Kuzichapa March 26 Manzese
Promota Jaffari Kitemo ‘katikati’
akiwainua mikono juu mabondia Ibrahimu Tamba kushoto na Said Mbelwa
wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana utakaofanyika March 26 Mwaka
huu katika ukumbi wa Frends Corner manzese Dar es salaam
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Ibrahimu Tamba na Said
Mbelwa jana wamesaini mkataba wa kuzipiga March 26 katika ukumbi wa
Frends Corner Manzese Dar es salaam mpambano huo wa raundi nane Kg 76 unaratibiwa na Jaffari Kitemo
Akizungumza mara baada ya
kutiliana saini mikataba ya kuzipiga Kitemo amesema kuwa siku Hiyo
kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ukiondoa pambano hili na Tumeandaa Mpambano uhu kwa ajili ya kuondoa ubishi wa nani zaidi mana
kila mmoja Anatamba mtaani kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie sasa jibu
tutalipata march 26 pale manzese
Nae bondia Mbelwa amesema kuwa kawaida yake ni kugawa dozi kwa kumpatia kipigo kitakatifu Tamba akijibu
majigambo hayo Tamba amesema kuwa yeye hana makuu hivyo Atahakikisha
anafanya mazoezi ya kutosha ili kumpiga mpinzania wake Mbelwa kwani
ngumi ni ngumi tu hazina msihara
No comments:
Post a Comment