Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa
mwaka wa mapitio ya sekta ya afya unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es salaam, wadau hao wa Sekta ya afya wanajadiliana mambo
mbalimbali na baada ya kumalizika kwa mkutano huo kutakuwa na kusaini
makubaliano yaliyofikiwa kwa utekelezaji katika sekta ya afya hapa
nchini , Katika picha kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika
ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Carol Hannon Mshauri wa Afya
katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania akizungumza katika mkutano huo
Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu.
Dk.Ulisubisya Mpoki Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
akichangia hoja katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.
Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu
wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano huo ambao umekutanisha
wadau wa afya na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya
afya.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano
unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano
unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………………………
Tamko La PamojaKuhusu Vipaumbele Vy Sekta Ya Afya Kwa Mwaka2016/2017
Na Kalonga Kasati
- KINGA NAa AFYA YA JAMII
Mwaka 2015 Serikali ya Tanzania
ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na kuanzisha mafunzo kwa kada
mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community Health Workers).
Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii huduma za afya za
msingi.
Mwaka 2016, Serikali ya
Tanzania itaendelea kutekeleza agenda ya huduma za Afya katika jamii
kwa kuhakikisha ubora wa mafunzo kwa wahudumu wa Afya ya Jamii,
kuendelea kuajiri wahudumu wa Afya ya Jamii na kufikisha huduma za Afya
za Kinga na tiba karibu zaidi na jamii.
- UWIANO
Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya
Afya (HSSP IV) umejielekeza zaidi katika uwiano na kusaidia maboresho
katika Sekta ya Afya katika maeneo ya pembezoni ambayo huduma za Afya
hazifiki kwa urahisi. Jambo muhimu katika hili ni kuendelea kusambaza
kwa uwiano rasilimali zote za kifedha zilizopo kutoka vyanzo vya ndani
na nje.
Ili kuhakikisha uwiano katika
mgawanyo wa rasilimali, ni muhimu kuwa na takwimu sahihi kuhusu uwepo wa
rasilimali kutoka vyanzo vya nje hususan wadau wa maendeleo, sekta
binafsi, mashirika ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali katika
ngazi ya wilaya.
Serikali itahakikisha kwamba
takwimu zilizopo zinaboreshwa kwa kukamilisha Mpango Kabambe wa kutambua
vyanzo vya nje vya mapato kwa mwaka 2016.
- UGHARAMIAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Mpango wa Afya kwa wote ni
kipaumbele cha Serikali ya Tanzania. Mkakati mpya wa ugharamiaji wa
Afya ulioandaliwa umeweka wazi njia ambayo Tanzania inaweza kutoa huduma
za Afya za uhakika wa kifedha kwa raia wote kupitia mfumo mmoja wa
Bima ya Afya ya Taifa.
Kwa mwaka 2016/2017, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itatafuta kibali
kutoka Mpango Mkakati wa ugharamiaji Afya na itaandaa hatua muhimu za
utekelezaji wa Mkakati ikiwa ni pamoja na kuhamasisha kupitishwa kwa
Sheria ya Mfuko Mmoja wa Kitaifa wa Bima ya Afya na kuleta pamoja
mitazamo mbalimbali ya Mfuko wa Afya ya Jamii.
Vilevile, wizara itafanya
uhamasishaji ili kuongeza rasilimali za ndani kwa ajili ya Sekta ya Afya
na kuongeza jitihada za Wizara mbalimbali katika kuboresha matumizi
yenye ufanisi wa rasilimali fedha zilizopo.
Wizara na Ofisi ya Rais- Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa zitaunda Mfumo rahisi wa utoaji taarifa
kuhusiana na mipango, bajeti na fehda, kwa ajili ya vituo vya utoaji
huduma za afya, ili kuwezesha ugatuaji wa kifedha kutoka wilaya kwenda
ngazi ya vituo vya afya.
- UTAWALA NA UONGOZI
Kuna miundo mbalimbali ya utawala
na uwajibikaji ndani ya Serikali na katika jamii inayofanya kazi katika
ngazi ya wilaya hususani katika masuala ya Afya kama vile Kamati za
Uongozi za Vituo vya Afya na zile zenye mamlaka makubwa zaidi kama vile
Kamati za Maendeleo za kata. Zote hizo zinajukumu la kuhakikisha
uwajibikaji katika utoaji huduma za Afya kwa wananchi.
Kwa mwaka 2016 Wizara, Ofisi ya
Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wadau wengine zitaweka wazi
mahusiano kati ya miundo hii katika ngazi ya wilaya kuhusiana na
Usimamizi wa Mipango, bajeti na fedha kwa ajili ya Afya. Vilevile ili
kuendeleza agenda ya ugatuaji, Wizara itashirikiana na Wizara ya Fedha
kusimamia mgawanyo wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma
za Afya.
- RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA AFYA.
Kuvutia na kuwezesha idadi kubwa
ya watumishi kuendelea na kazi katika utoaji huduma bora za Afya hususan
katika maeneo ya vijiji na maeneo ambayo huduma za Afya hazifiki kwa
urahisi, ni changamoto nchini Tanzania, maendeleo ya kuridhisha
yamefanyika kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa na Program nyingine.
Ili kuendeleza zaidi mafanikio
yaliyofikiwa, mwaka 2016 Wizara, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zitaendeleza
Sera ya mabadiliko yanayohitajika ili kutekeleza mpango wa mabadiliko
makubwa sasa (BRN) kuhusiana na rasilimali watu katika nyanja za afya na
zitashirikiana na Serikali za Mitaa kuwezesha utekelezaji wa Sera ya
Malipo na motisha.
Ili kuhakikisha upatikanaji wa
huduma bora za afya, Wizara itakamilisha mwongozo wa kushirikiana katika
majukumu, kuweka wazi majukumu ya kila kada na kukamilisha mwongozo wa
kujiendeleza kitaaluma.
- DAWA, VIFAA NA VIFAA TIBA
Uboreshaji wa usimamizi na
utawala wa Dawa, vifaa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za
afya hususan katika ngazi ya wilaya ni kipaumbele chini ya Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa na Mpango wa Nne wa HSSP.
Matatizo ya kifedha yana maanisha
kwamba rasilimali zilizopo hazina budi kutumiwa kwa ufanisi na namna
nyingine za ugharamiaji wa dawa na vifaa vingine muhimu hazinabudi
kutafutwa. Ili kuhakikisha haya yanafanyika, mwaka 2016 Wizara
itajielekeza katika kuboresha utendaji na ufanisi wa Bohari Kuu ya Dawa
(MSD) ikiwa ni pamoja na kuwezesha ulipaji wa deni.
Kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
– Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara vilevile itahakikisha
rasilimali zilizopo na nyingine mpya kwa ajili ya usambazaji wa vifaa
zitaelekezwa katika vipaumbele vya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa na
itatoa miongozo sahihi ya Kisera inayoainisha Mfumo mmoja wa ununuzi wa
dawa na vifaa tiba muhimu itakayofuatwa na mamlaka ya Serikali za Mitaa
na vituo vya kutolea huduma za Afya.
- UFUATILIAJI, TATHMINI NA USIMAMIZI WA TAKWIMU
Maboresho mengi yamefanywa katika
mfumo wa usimamizi wa takwimu kwenye Sekta katika miaka ya hivi
karibuni, hata hivyo bado kuna changamoto hususan kwa upande wa
uhamiaji kwenda katika Mfumo wa kielektroniki na matumizi ya takwimu
katika utoaji wa matumizi.
Uwepo wa takwimu sahihi utasaidia wilaya kupanga vizuri matumizi yao.
Wizara imedhamiria kukamilisha
Mpango wa kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya huduma za afya kufikia
mwisho wa mwaka 2016, ikiwa ni pamoja na kuhama kutoka mfumo wa
kutumia karatasi kwenda mfumo wa kielektroniki na pia katika kuongeza
uwezekano wa kuunganisha mifumo ya takwimu.
Ili kuendeleza dhana ya utoaji
uamuzi unaotokana na ushahidi, Wizara itashirikiana na Ofisi ya Rais –
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika masuala ya takwimu muhimu
zinazotokana na mamlaka za Serikali za Mitaa na watumiaji wengine kwa
wakati katika mfuko rafiki unaowezesha utoaji wa taarifa za mipango na
utoaji wa maamuzi.
- UTOAJI HUDUMA
Mwaka 2015 Wizara ilianzisha Mfumo wa tathmini wa vituo vya msingi vya utoaji huduma za afya.
Mfumo nyota ambao unazingatia
vigezo vya ubora wa huduma (quality of service) za madaraja katika
kuanzisha viwango vya utoaji huduma. Mwaka 2016 Wizara kwa
ushirikiano na TAMISEMI itahakikisha kwamba tathmini ya Matokeo ya
nyota inatafsiriwa katika uboreshaji huduma katika vituo na kwamba
ugharamiaji unawekwa katika Mpango Kabambe wa Afya wa kituo na
Halmashauri. Mfumo nyota unaonyesha vituo katika kazi mkoa, rufaa na
Taifa utakamilika 2018.
Vilevile, Wizara itaipitia miongozo iliyopo ya usimamizi ili kuainisha majukumu ya ukaguzi na usimamizi.
UZINDUZI WA MPANGO MKAKATI WA NNE WA SEKTA YA AFYA 2015-2020
Utangulizi
Mpango mkakati wa nne (HSSPIV) ni
mpango ulioandaliwa kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta ya Afya
ikiwa ni pamoja na Serikali, Wadau wa Maendeleo, Sekta binafsi, taasisi
za kijamii na Ustawi wa jamii.
Lengo kuu la mpango huu ni :kufikisha huduma bora muhimu za Afya na Ustawi wa jamii katika ngazi za kaya zote nchini.
Mpango unaainisha Mikakati mitano:
1.Kuboresha kiwango cha Ubora wa
huduma katika ngazi zote za afya ya msingi kwa kuhakikisha kuwa kila
mwananchi anafikiwa na kitita bora cha afya na ustawi wa jamii
- Kuboresha Uwiano wa upatikanaji wa huduma bora za afya na ustawi wa jamii kwa kuondoa tofauti zilizopo za kijografia, kiuchumi na makundi maalum kama vile wazee, watoto, wajawazito na walemavu.
- Kuboresha Ushirikishwaji wa jamii katika kupanga na kusimamia huduma za Afya na Ustawi wa jamii. Hii inajumuisha uhamasishaji wa mifuko ya afya ya jamii, usimamiaji wa vituo vya huduma, uwepo wa dawa vituoni, utambuzi wa wasiojiweza ili wapate huduma, na uwajibikaji wa watoa huduma kwa wanajamii husika.
4.Uwekezaji katika mikakati na njia za kisasa na ubunifu
kama : Ugharamiaji
-Mkakati wa Bima moja ya Afya kwa wote
-Ushirikiano na sekta binafsi
-Ushirikiano wa wadau wote wa sekta ya afya maendeleo na ustawi waj amii.
5.Kutambua Ushiriki wa jamii na
Sekta nyingine katika afya. Afya bora siojukumu la wizara moja; Hii
inajumuisha uhamasishaji wa wa kila sekta kuwa na mkakati wa Afya. Hii
itasaidia kushughulikia mambo muhimu kama; Lishe na afya za watoto,
Maji safi, elimu ya afya, Usafi wa mazingira, umuhimu wa barabara na
mawasiliano katika dharura ya kiafya na itapunguza magonjwa kama
kipindupindu, vitambi, presha
No comments:
Post a Comment