CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU IRINGA (IRFA) KUJENGA UWANJA WA KISASA
Kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza ofisini kwake
mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava
alisema wameamua kujenga uwanja wao ili kuepukana na adha wanayopata
kutokana na kukosa sehemu ya kuendeshea ligi mbalimbali .
Alisema tayari wameshapata eneo
la hekari 14 katika eneo la kitwiru ndani ya manispaa ya Iringa Na sasa
kinachosubiriwa ni kumaliza mazungumzo kati ya chama hicho na manispa
ya Iringa ili kuweza kumilikishwa eneo hilo ili liwe mali yao kabisa
tofauti na apo awali ambao manispaa hiyo ilikuwa inataka kuingia nao
ubia
“Tayari hili swala liko katika
hatua za mwisho na tayari tumesha fanya mazungumzo tunataka Tujenge
uwanja wetu wenyewe wa kisasa ambao tunaweza kucheza mechi za kimataifa
kwani Tumekuwa tukipata tabu ya viwanja vya kuchezea na hii imechangia
kwa kiasi kikubwa kuuwa soka la mkoa wetu ”alisema Kuyava
Alisema wanasubiri majibu ya
maombi waliyopeleka katika manispaa hiyo ili kuweza kupunguziwa Bei li
kuanza mchakato wa kulipa fidia kwa wamiliki wa maeneo hayo ili waanze
mchakato wa uwanja huo wa kisasa .
Alisema kuwa mara nyingi timu
zimekuwa hazi pati kitu wanapotumia viwanja vya watu kwani Asilimia 16
za mapato yanayopatikana kutokana na kingilio huchukuliwa na wamilika
wa kiwanja Na asilimia ndogo inabaki ndio zinagawanywa katika maeno
mengine na kujikuta timu hazinufaiki na chochote .
Alisema kuwa hapo awali walikuwa
wakitumia uwanja wa samora ambao bado uko katika Matengenezo tena ya
kusuasu kwa kuwa mpaka sasa bado wanadai kusubiri nyasi za kupanda Jambo
litakalorudisha michezo nyuma endapo hawatakuwa na maono ya kuwa na
kiwanja chao wenyewe .
Kwa upande wa wadau wa soka mkoa
wa Iringa Ally salehe ambaye pia ni shabiki wa timu ya lipuli Anasema
kuwa endapo juhudi za makusudi zitafanyika na kufanikisha ujenzi wa
uwanja huo basi ni dhahiri kuwa soka la mkoa wa iringa litapanda kwa
kiasi kikubwa .
No comments:
Post a Comment