Ligi Daraja la Pili (SDL) nchini
inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu zote 24 kucheza katika
viwanja mbalimbali, kusaka timu nne za juu kutoka kila kundi
zitazokpanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Jumapili Kundi A, Mvuvumwa FC
watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini
Kigoma, Mirambo FC watacheza dhidi ya Green Warriors uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora, huku siku ya jumatatu Abajalo Tabora
wakichuana dhidi ya Transit Camp katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Kundi B, Jumapili Pamba FC
watacheza dhidi ya Alliance Schools uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma
watawakaribisha AFC ya Arusha kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma, huku
siku ya Jumatatu Bulyanhulu FC wakicheza dhidi ya Madini FC kwenye
uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kundi C, Jumatatu Mshikamano
watawakaribisha Cosmopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam,
Karikaoo FC watawakaribisha Villa Squad uwanja wa Ilulu mjini Lindi,
huku Changanyikeni wakicheza dhidi ya Abajalo Dar kwenye uwanja wa
Karume jijini Dar es salaam.
Kundi D, Kesho Jumamosi African
Wanderes watawakaribisha The Mighty Elephant uwanja wa Wambi Mafinga,
Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Sabasaba, huku Wenda FC
wakicheza dhidi ya Mbeya Warriors katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
MalinziAmpongeza Mwenda Wa FKF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Rais
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya (FKF), Nick Mwendwa
kwa kuchaguliwa kuliongoza shirikisho hilo.
Katika salamu hizo, Malinzi
amempongeza Mwendwa kwa nafasi hiyo aliyopewa kuliongoza soka la nchini
Kenya, na kuahidi TFF itaendelea kushirikiana nae katika maendeleo ya
mpira wa miguu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Nick Mwendwa alishinda nafasi
hiyo jana katika uchaguzi uliofanyika jijini Nairobi kwa kupata alama 50
kati ya 77 za wapiga kura wote na kupata nafasi hiyo iliyokua
inashikiliwa na Samwel Nyamweya aliyemaliza muda wake.
Startimes League KumalizikaWikiendi Hii
Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes
League) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa kwa
wakati mmoja katika viwanja mbalimbali nchini, huku Kundi A na C
zikisaka vinara watakaopnda Ligi Kuu msimu ujao.
Bodi ya Ligi (TPLB) imeviandikia
barua vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi hiyo, wasimamizi wa vituo
kuwafahamisha kuwa mechi zote zinatakiwa kuchezwa kwa muda mmoja na
kusisitiza kuwa mechi zote zitaanza saa 10 kamili jioni bila kujali kama
jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Ni jukumu la Msimamizi na
Kamishna kuhakikisha mechi yake inaanza katika muda uliotajwa (saa 10
kamili) bila kukosa. Utekelezaji wa maelekezo haya ni muhimu ikiwa ni
moja ya njia ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya upangaji wa matokeo
vinavyoweza kujitokeza.
Mechi za mwisho za Kundi A hatua
ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Friends
Rangers FC vs Kiluvya United FC (Mabatini), Polisi Dar vs Polisi Dodoma
(Shirika la Elimu Kibaha), Ashanti United vs African Lyon (Karume) na
Mji Mkuu vs Kinondoni Municipal Council FC zitachezwa Februari 14, 2016
katika viwanja husika.
Mechi za mwisho za Kundi B hatua
ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Kimondo Super
SC vs Kurugenzi FC (Vwawa), Njombe Mji vs Lipuli FC (Amani), Ruvu
Shooting vs Polisi Morogoro (Mabatini) na Burkina FC vs JKT Mlale
(Jamhuri) zitachezwa Februari 13, 2016.
Mechi za mwisho za Kundi C hatua
ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Mbao FC vs
Polisi Mara (CCM Kirumba), Polisi Tabora vs JKT Oljoro (Ali Hassani
Mwinyi) na JKT Kanembwa vs Geita Gold (Lake Tanganyika) zitachezwa
Februari 13, 2016 katika viwanja husika.
No comments:
Post a Comment