Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 waliofukuzwa CUF
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017
imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa
uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba
ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.
Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia
mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa
mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza
kuapishwa.
No comments:
Post a Comment