Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa kushoto
akikabidhi msaada wa mabati kwa ajili ya kuweka uzio katika uwanja wa
mpira ulipo katika shule ya msingi Muhoro Wilayani Rufiji Mkoa wa
Pwani,(PICHA NA VICTOR MASANGU
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akisalimiana na wazee maarufu ambao ni wadau wakubwa wa mchezo wa kandanda waliohudhuria sherehe hizo katika kijiji cha muhoro mara baada ya hafla fupi ya kukabidhi mabati 650 kwa ajili ya kuweka uzio katika uwanja wa mpira uliopo shule ya msingi muhoro(picha na Victor Masangu)
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
Mbunge wa jimbo la Rufiji
Mohamed Mchengerwa katika kuunga juhudi za serikali katika kuboresha
viwanja vya mpira ametoa msaada wa mabati 650 kwa ajili ya kuweza kuweka
uzio ambao utaweza kusaidia kuingiza ukusanyaji wa mapato pamoja na
kukuza na kuviendeleza vipaji vya mchezo wa soka kwa vijana.
Akikabidhi msaada huo wa mabati
650 katika hafla iliyofanyika katika uwanja huo wa mpira wa shule ya
msingi Muhuro Mchengerwa aliesema kwamba uwanja huo umekuwa ukitumika
katika mashindano mbali mbali lakini changamoto kubwa ilikuwa hakuna
uzio.
Mchengerwa alionngeza kuwa
lengo lake kubwa ni kuona katika jimbo lake vijana wote wanashiriki
kikamilifu katika michezo ili kuweza kupata wachezaji wenye vipaji
ambao wataweza kuchezea hata timu ya Tiafa katika siku zijazo.
“Mimi kama mbunge a jimbo la
Rufiji nia yangu kubwa ni kuhakikisha kwamba ninawekamikakakti kabambe
ya kuwaendeleza vijana katika suala zima la michezo, na ndio maana
nimeona kuna umhumihu mkubwa katika uwanja huu kuuzungushia uzio wa
mabati, ili pindi ligi mbali mbali zinapofanyika kuweze kuwa na
kiingilio ili fedha zitakazopatikaka ziweze kusukumu gurudumu ya
kuendeleza michezo,”alisema Mchengerwa.
Aidha alibainisha kwamba wakati
alipokuwa katika mchakato wa kampeni zake aliwaweza kuahidi kuleta
mabadiliko chanya katika sekta ya michezo kuanzia ngazi zote z vijiji
hata ngazi ya Wilaya ikiwemo sambamba na kuboresha viwanja ambavyo vipo
katika jimbo lake la Rufiji.
Pia alisema katika ktimiza azma
yake ya kufufua vipaji kwa vijana na kuviendeleza endeleza anatarajia
kuanzisha mashindano makubwa ya mchezo wa soka ambayo yatazishirikisha
timu mbali mbali kutoka kata zote 13 zilizopo katika jimbo lake.
Katika hatua nyingine Mchengerwa
aliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuweka utaratibu wa kwenda
kutembelea timu zilizopo katika maeneo ya vijijina kwani kuna vijapi
vingi ambavyo vinashindwa kuonekana kutokana na kutokupata sapoti ya
kutosha hivyo kusababisha kukokosa wachezaji wazuri ambao wanatokea
ngazi za chini.
“Hapa kwa hili pamoja na
kuendeleza na juhudi za ngungu za kuendeleza vijaji vya wachezaji lakini
TFF, ambao ndio wasimamizi wa mchezo huu wa soka kulianagalia suala
hili kwa jicho la tatu, hususan kwa upande wa wachezaji wa ngazi za
chini, kwani mimi nimeweza kubaini kuna wachezaji wengi wazuri sana ila
changamoto wanajikuta wanakosa sapoti na kuwepo kw achangamoto ya
viwanja,”alisema Mchengerwa.
Katika hatua nyingine aliongeza
kwamba katika kukuza sekta ya michezo atahakikisha kwamba kwa sasa
anaweka program maalumu kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo
wa soka ili kuweza kuwasaidia wachezaji wenye vipaji, sambamba na
kuwapatia vifaa mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kufanya
mazoezi.
No comments:
Post a Comment