Waumini wakiwa mbele ya vibanda vya biashara vilivyopo nje ya msikiti huo. |
Watoto wa shule ya awali katika msikiti huo wakiwa na mwalimu wao (kulia)
Na Kalonga Kasati
TAFRANI
kubwa imezuka katika Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja
Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa msikiti huo
kudaiwa kutafuna zaidi ya sh.milioni 20.
Fedha
hizo imeelezwa kuwa zilichangwa na waumini wa msikiti huo kwa ajili ya
ujenzi wa msikiti mpya baada ya unaotumika kuchakaa.
Imamu
mkuu wa msikiti huo aliyetajwa kwa jina la Hamidu Mitanga alilazimika
kutoweka ndani ya msikiti huo baada ya kuendesha swala ya Ijumaa
iliyofanyika jana mchana kutokana na waumini kuwa na jaziba kufuatia
imamu huyo kutamuka kuwa hakuhitaji kuulizwa maswali yoyote kuhusu
upotevu wa fedha hizo na kuwa uongozi uliopo utaendelea kuwepo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi msikitini hapo Dar es Salaam leo mchana
wakati wa swala ya Ijumaa mmoja wa waumini wa msikiti huo Mbarouk
Mohamed Makame alikiri kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za waumini
zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
“Suala
la upotevu wa fedha hizo lipo na limeleta changamoto kubwa kwa waumini
na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa lile
linalolalamikiwa kutafuna fedha hizo na lile linalotaka fedha hizo
zitolewe maelezo zilipo” alisema Mzee Makame.
Mzee
wa msikiti huo na Mwenyekiti wa Kamati ya watu 10 Saidi Ngubi alisema
fedha zinazoshindwa kutolewa maelezo ya matumizi yake na viongozi wa
msikiti huo zilitokana na mradi wa maji na michango ya waumini.
“Mimi
ndiye niliyeanza kuuliza matumizi ya fedha hizo lakini viongozi hao
wakawa hawana majibu na badala yake waliivunja kamati yetu na kuchagua
nyingine jambo lililoleta sintofahamu” alisema Ngubi.
Imamu
mkuu wa msikiti huo Hamidu Mitanda alisema fedha hizo zilitumika kwa
ajili ya mchakato mzima wa kupata umiliki wa kiwanja ulipo msikiti huo
na michoro ya ujenzi wa msikiti mpya na kuwa yeye ndiye aliyeanzisha
mpango wa kupata msikiti ulio bora na si bora msikiti.
“Binafsi
sina shida na cheo hiki cha Uimamu kwani nina shughuli zangu nyingi
mkitaka kuniondoa fuateni taratibu kama zili zilizoniweka madarakani na
sisi kama viongozi dhamira yetu ni kuwa na msikiti uliobora wa ghorofa
na si bora msikiti” alisema Mitanga.
Mitanga
alisema chokochoko hizo zilianza tangu mwaka 2007 ambapo tulikubaliana
kila muumini kati ya waumini 205 achangie sh.5000 za ujenzi lakini
waliochangia walikuwa ni waumini wachache ambapo zilipatikana sh.milioni
moja tu.
Imamu
huyo alisema uongozi unaoendesha msikiti huo hauko tayari kuachia
madaraka kwa tuhuma hizo ambazo hazina ukweli alizodai zinachochewa na
baadhi ya waumini.
Zantel yaipa maktaba kuu 10 m/- kununulia vitabu
Na Salum Vuai-Zanzibar
KAMPUNI ya simu Zantel,
imeendelea kuipa msukumo sekta ya elimu Zanzibar, mara hii ikitoa msaada
wa shilingi milioni kumi kwa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar kwa
ajili ya kununulia vitabu na uendeshaji wa shughuli zake.
Akizungumza katika hafla
iliyofanyika leo katika jengo la maktaba hiyo Maisara mjini Zanzibar,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Benoit Janin, amesema msaada huo
unalenga kusaidia upatikanaji wa maarifa miongoni mwa jamii ya
Wazanzibari.
Janin alisema, ni miongoni mwa
majukumu na wajibu wa Zantel, kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye
ufanisi zinazokidhi mahitaji ya wakaazi wanaoishi mijini na vijijini na
kurahisisha upatikanaji wa taarifa za elimu, habari, utamaduni na
burudani.
“Upatikanaji wa maarifa kwa
wanajamii ni jambo la muhimu na suluhisho la changamoto hii ni
kuhakikisha tunatoa fursa sawa kwa kuwezesha kukua kwa maktaba za
jamii,” alisema Janin.
Aidha alieleza kuwa, ni fahari
kwa kampuni yao kusaidiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa
kuchangia ukuaji na ustawi wa jamii.
“Tunaamini kwamba kujifunza ni
muhimu kwa maendeleo ya elimu kama moja maeneo ya shughuli zake za
kusaidia jamii,” alieleza Ofisa huyo.
Akitoa shukurani zake kwa Zantel,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee,
aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao wa miaka mingi katika kukuza
maendeleo ya elimu Zanzibar.
“Tunafarijika na mchango wa
Zantel katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini, na msaada huu
uliotolewa leo kwa maktaba yetu kuu utasaidia kurahisisha upatikanaji wa
vitabu na hivyo kuimarisha mazingira ya utoaji maarifa miongoni mwa
Wazanzibari,” alieleza.
Hata hivyo, aliiomba kampuni hiyo
kuangalia uwezekano wa kusaidia maeneo mengine ya kielimu
yanayokabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kukamilisha ujenzi wa
baadhi ya madarasa uliokwama, pamoja na madawati.
Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar Sichana Mussa Foum, aliishukuru
Zantel kwa msaada huo, akisema ni muhimu kwa wateja wa maktaba zake
Unguja na Pemba.
Alifahamisha kuwa, pamoja na
jitihada za serikali kuziendeleza maktaba hizo, mchango wa taasisi
nyengine unahitajika kutoana na ongezeko la wanafunzi na wananchi
wanaohitaji huduma za maktaba.
WAZIRI ANASTAZIA WAMBURA AKUTANA NA TFF
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura leo ametembela ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata kujionea shughuli
mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso hilo.
Akiongea na viongozi na wachezaji
wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” waliopo kambini kujiandaa na
mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake
dhidi ya Zimbambwe, Wambura amesema Serikali itashirikiana na TFF
kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo wa awali utakaochezwa
Machi 4, 2016.
Wambura amewataka wachezaji wa
Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja, kujituma na
kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni ajira itakayoweza kuwasaidia
kuendesha maisha yao.
Aidha Wambura amesema anaamini
kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo
unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi kuhakikisha inapanda na
kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la wanawake.
Pia amesema wizara yake
inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya TAMISEMI ikasimishe mchezo
wa mpira wa miguu katika mashindano ya UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze
kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye utaalamu wa mchezo huu.
No comments:
Post a Comment