Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa na
aliyekuwac Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo kwa sasa ni mgombea Jimbo la
Kikwajuni Uwakilishi Mhe Nassor Salim Jazira akiwa katika ziara hiyo ya
Mhe Waziri Zanzibar
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Eng Hamad Yussuf
Masauni akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Jangombe Ali Hassan Omar King
wakiwa katika ziara hiyo kutembelea miradi ya Muungano ya Tabia Nchi
Zanzibar.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi akitowa maelezo jinsi eneo
hilo la kilimani lililoathirika na Tabia Nchi Zanzibar likiwa chini ya
mradi wa Kujenga Uwezo wa Jamii Kuhimili Mabadiliko Tabia Nchi
(LDCDF)kilimani kwa Upandaji wa Mikoko na Uwekaji wa Matuta kuzuiya
Mmomonyoko wa Ardhi katika Ukanda wa Bahari.
Eneo ambalo limekumbwa na Tabia nchi katika kilimani likiwa limejaa maji ya pwani
Naibu
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe
Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake ya kutembelea miradi ya kuhifadhi
mazingira Zanzibar akitembelea moja ya mradi huo ulioko kilimani
Zanzibar kujionea jinsi ya hali ya uharabifu wa Tabia Nchi katika eneo
hilo.
Ujumbe wa Maafisa wa Mazingira wa Afisi ya Rais Muungano wakitembelea eneo hilo na Naibu Waziri Mhe Luhaga Mpina.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Masauni akiwa katika ziara hiyo
kutembelea eneo hilo la kilimani lililoharibika kwa kuliwa na bahari
kutokana na Tabia Nchi.
Eneo
la Ufukwe wa Kilimani uliovyoliwa na Tabia Nchi kama unavyoonekana
pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe
Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na
Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo
la kilimani Zanzibar.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe
Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na
Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo
la kilimani Zanzibar.
Sheha
wa Shehia ya Kilimani akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na
Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitowa maelezo ya eneo mpja lililoathirika
na Tabia nchi katika eneo la kilimani akimuonesha uliokuwa uwanja wa
kilimani Stars kwa sasa uwanja huo umekuwa ni sehemu ya kukaa maji ya
bahari wakati wa maji kujaa. na kufika karibu na sehemu ya makaazi ya
wananchi.
Naibu
Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina akitembelea
eneo hilo wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Tabianchi Zanzibar
akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni
Zanzibar wakiwa kastika ufukwe wa pwani ya kizingo.
Naibu
Waziri wa Afisi ya Rais Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina
na Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nadi Mhe Eng Hamad
Yussuf Masauni wakitembelea eneo la ufukwe wa pwani ya kilimani
ilioathirika kwa kuliwa na bahari sehemu kubwa ya eneo hilo na kuingia
maji katika maeneo ya jirani na makaazi.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kudhibiti tabia nchi kwa
eneo hilo la kilimani na kuharibu sehemu kubwa ya eneo hilo ambalo
lilikuwa na uwanja wa mpira na kuliwa na bahari.
Naibu
Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga
Joelson Mpina akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea
eneo hilo lililokubwa na athari za Tabia nchi katika pwani ya ufukwe wa
kilimani na kuagiza kupandwa kwa mikoko katika eneo hilo ambolo ifikapo
mwezi wa marchi na fedha zake zipo kwa kazi hiyo na zoezi hilo limeaza
mwezi huo kwa kuaza kwa kupandwa kwa miti ya mikoko na ujengaji wa tuta
la kuzuiya maji ya bahari kuendelea kula eneo hilo ambalo tayari
limeharibia na maji ya bahari.
Naibu
Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe
Luhaga Joelson Mpina Naibu Waziri wa Mambi ya Ndani na Mbunge wa Jimbo
la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mbunge wa Jimbo la Jangombe
Mhe. Ali Hassan Omar King wakitembelea eneo la pwani ya kilimani
lililokumbwa na athari za TabiaNchi. wakati wa ziara yake Kisiwani
Zanzibar
No comments:
Post a Comment