Wednesday, 3 February 2016

Mkoa Mpya Songwe Na  Wilaya Mpya Zaanzishwa

indexWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya waSongwe na Wilaya sita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.
Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.

Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

“ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.

Matukio katika picha Bungeni Dodoma Leo

1
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge pamoja na  Waziri wa Nchi Ofisi Utumishi na utawala Bora Mhe.Angellina Kairuki wakiwasili katika viwanja vua Bunge kwa ajili ya kushiriki kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
2
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge akiwasili katika ukumbi wa Bunge tayari kwa kuongoza kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
4
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge akiongoza sala kwa ajili ya Bunge na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
5
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge Kazi, Vijana na Ajira Mhe Anthony Mavunde akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
6
Waziri wa Nchi Ofisi Utumishi na utawala Bora Mhe.Angellina Kairuki akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
7
Wairi wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe dkt Hussein Mwinyi akiteta jambo na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
8
Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.prof Makame Mbalawa akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
9
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.George Masaju  akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma

No comments:

Post a Comment