Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.
Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo
pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao
waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na
uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo
kitengo cha maabara.
Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.
Kaimu
Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa
fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na
wafanyakazi katika mkutano wake huo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake…
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla
akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa
kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua
kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa
hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo
kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo
Februari 12.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata
maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda
ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana
hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe
mpya ilikuendana na kasi.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa
malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu
Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo
imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla
amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya
Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo
upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa
endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa
watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na
kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji
kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja
na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa
Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla
alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD),
Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo,
wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo
kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa
Hospitali.
Dk.Kigwangalla
alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile
linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto
zinazowakabili.
“Hospitali
kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya
biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande
wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?” alihoji Dk. Kigwangalla.
Dk.Kigwangalla
aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya
jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya
bima ya afya.
Aidha, Dk Kigwangalla amewataka
uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo
kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za
wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.
MuonekanoWaKituo Kipya Cha Kusuma Maji Ruvu Darajani Kikiwa Kimekamilika
Muonekano
wa kituo kipya cha kusukuma maji kilichopo eneo la Ruvu Darajani kikiwa
kimekamilika ambapo kitakuwa kinasukuma maji kwenda katika mtambo wa
Ruvu Juu.
Pampu moja ya kituo hicho inauwezo
wa kusukuma maji lita milion 60 kwa siku kuna jumla ya pampu mpya tatu
na pampu mbili zitakuwa zinafanya kazi kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment