Wednesday, 3 February 2016

Dk. Salim Kuzindua Kituo Cha Utafiti ChaMafunzoYa Uyoga Cha Chuo Kikuu Cha Kairuki

 Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia Februari 4. Kushoto ni Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
 Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert
Kairuki yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu
ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni. 
 
Na Kalonga Kasati
 
Katika  kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu  cha  kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia Tarehe  4 hadi  6 Feb ambayo  itakuwa ni siku  ya kilele.Mh Dr Salmin
Ahmed Salim  ambaye  pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la
Utafiti  na  mafunzo ya Uyoga  lililopo huko  Boko katika eneo la chuo hicho.

Sambamba na uzinduzi huo  pia shughuli  nyingine katika  kumbukizo hizo  itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na
Profesa  Keto  Mshigeni  ambaye ndiye  makamu mkuu  wa Chuo hicho  na mwanasayansi aliyebobea katika  tafiti  za uyoga.

Pia  hospital  ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya
macho  bila  ya malipo kwa siku  mbili  mfululizo.

Pia patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo  ya
saratani ya kizazi.

Aidha  wanafunzi wa zamani wa chuo  hicho waliopo  Mwanza  na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha
kumbukizo hizo  kwa  kufanya  zoezi la kupima afya
bure  kwa wakazi  wa huko.

Wananchi wahimizwa kujitokeza kupima Saratani.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani .
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani.
 
 
Na Tabu Mullah
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wanatarajia
kutoa  elimu, huduma na vipimo vya  bure vya magonjwa ya saratani ili kuiwezesha jamii
kujikinga na ugonj
wa huo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatano) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa  Wizara hiyo, Dkt. Ulisubisya Mpoki huduma hizo za matibabu na vipimo vitaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya saratani
duniani inayoathimishwa ulimwenguni kote tarehe 4. Februari ya kila mwaka.
Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika
katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda
kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi
dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza
Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya
saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri
ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi
ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho yaSiku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA
JANGA LA SARATANI DUNIANI.”

No comments:

Post a Comment