Saturday 2 May 2015

MWAMASISHAJI YA MAUAJI YA A.KUSINI HUYU HAPA

 

WAKATI dunia ikiendelea kulaani mauaji ya wageni yanayoendelea nchini Afrika Kusini. Kauli ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe imeanza kugeuzwa kuwa mtaji wa kisiasa nchini Tanzania. Waziri Membe katika taarifa yake juu ya usalama wa watanzania walioko nchini humo, alisema kwamba Serikali imejipanga vizuri ili kuwarudisha watanzania
walioko Afrika ya Kusini. "Sio wote wanaovamiwa, wavamizi Wakikuuliza unatokea wapi na ukawaambia kuwa wewe ni Mtanzania hawakugusi!' 'Xen ophobia is Selective Not all people are subjected to violence When they ask you where are you from and you tell them that you are a Tanzanian they don't touch you"Said Hon Membe. Katika hatua nyingine Waziri Membe alisema kwamba pamoja na kwamba wanasubiri taarifa kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini lakini pia aliwataka watanzania kuacha kuwa na wasiwasi zaidi kwa sababu mauaji hayo yanalenga watu wa mataifa mengine na si Watanzania. Membe alisema kwamba wauaji wanauliza kwanza utaifa wa mgeni na kwamba wakiwambia kwamba wewe ni mtanzania wanakuacha. Hata hivyo wakati taarifa ya Membe ikidai kwamba mauaji hayo hayawalengi watanzania na kwamba mpaka hivi sasa hakuna mtanzania aliyeuwa katika vurugu hizo, taarifa zaidi zinadai kwamba kuna watanzania watatu wameuawa katika vurugu hizo.Waziri Membe alikanusha taarifa hizo vikali na kudai kwamba watanzania hao hawakuuawa katika vurugu hizo bali vifo vyao vilitokana na sababu mbalimbali. Membe alisema kwamba ni watanzania 21 tu ambao ndio wamekubali kurudi nchini kati ya watanzania 23 waliokimbia machafuko yanayowakumba wageni nchini Afrika ya Kusini na kuhifadhiwa kwenye kiwanja kimoja cha mpira kilichopo nchini humu. Serikali itawarudisha watanzania ambao wamepata matatizo ya kuvamiwa ambao tayari serikali imeshawatambua. Hata hivyo Membe alizema kwamba kamwe Serikali haitamrudisha Mtanzania yeyote ambaye atatumia machafuko hayo yanayoendelea nchi umo kama njia ya kurudi Tanzania, ambapo amedai kuwa wapo Watanzania wengi wamekuwa wakihangaika na maisha wakitaka kurudi nyumbani na kudai kuwa serikali haitoweza kuwarudisha wote kwani wako wengi sana wanaishi huko. Amebanisha kuwa jambo ambalo serikali inasubili kwa sasa ni kupata ruhusa kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania alioko Afrika ya kusini ili kuwarejesha watanzania hao waliokubali kurudi nchini.Katika hatua nyingine Waziri Membe amekanusha Vikali taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kwenye Mitandao ya Kijamii pamoja na baadhi ya magazeti wakidai kuwa watanzania watatu wamefariki kutoka na machafuko hayo. "Taarifa hizo ni za uongo kwani Watanzania hao watatu wamekufa kutokana na magonjwa mbali mbali na sio sababu ya machafuko hayo". Membe amewataja watanzania hao ni Athumani China ambaye anasema mtanzania huyo amekufa kutokana na kupigwa na wananchi wa nchi hiyo baada ya kumpora mwenyeji wa huko. Mwingine ni Ally Mohamed ambapo pia amesema huyo naye amefariki kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kifua kikuu,pamoja na mtanzania mwingine aliyekufa gerezani alipofungwa ambapo alikufa kutokana na kuchomwa visu. Vilevile Waziri Membe akawataka watanzania waishio nje ya nchi kupenda tabia ya kuwa pamoja ili matatizo kama hayo yaliyotokea Afrika ya Kusini yakiwakuta popote iwe raisi kwa Serikali kutoa msaada.

No comments:

Post a Comment