Saturday 16 May 2015

Maalim Seif asema Zanzibar itashinda vita dhidi ya uzalilishaji

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema Zanzibar itashinda vita dhidi ya udhalilishwaji wa wanawake na watoto iwapo kutakuwa na nguvu ya pamoja kati ya serikali, jumuiya za kiraia na jamii katika kuvitokomeza vitendo hivyo.
Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar, waliofanya naye mazungumzo huko nyumbani kwake Mbweni mjini Unguja, kuhusiana na shughuli wanazozifanya.
 
Alisema mbinu muafaka ya kutokomeza vitendo hivyo ni kufanyika utafiti wa kina ili baadaye wadu wote wakiwemo polisi, mahakama, viongozi wa dini, wana jamii na serikali kuwekewa mkakati maalum katika kufanikisha wajibu wa kila upande.
 
Maalim Seif alisema hali ya udhalilishwaji wanawake na watoto Zanzibar imefikia katika kiwango cha kutisha na ni lazima hatua zinazochukuliwa na taasisi mbali mbali, kikiwamo Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa), Zanzibar ziungwe mkono.
 
Alikipongeza chama hicho Zanzibar kutokana na kazi nzuri ya kupigiwa mfano kwa kuelimisha jamii kukomesha vitendo vya udhalilishwaji wanawwake na watoto.
 
“Kuishawishi jamii na hasa wanaume waachane na vitendo hivi si kazi rahisi, lakini nyinyi mnaifanya kwa ufanisi, nadhani hatua mliyofikia sasa ni ya mafanikio makubwa,” alisema Maalim Seif.
 
Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa, alisema mbali na kupiga vita vitendo vya udhalilishwaji, Jumuiya hiyo inaendelea na juhudi za kuwajengea uwezo wanawake wa Zanzibar katika maeneo tafauti, ikiwemo kuwawezesha kushika nafasi za maamuzi, ikiwemo Ubunge na Uwakilishi.
 
Alisema mbali na wanawake kuonesha uwezo mkubwa katika kusimamia majukumu, wapo wanaoshika nyadhifa mbali mbali, lakini wamekuwa wakipambana na vikwazo vigumu wanapoamua kuwania nafasi za kisiasa kupitia vyama.
 
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake (UN Women), Ali Sultan, akizungumza katika hafla hiyo alisema miongoni mwa hatua wanazozichukua ni kuwapa ujasiri na kuwaondolea hofu wanawake kwa azma ya kuwawezesha kuwania nafasi mbali mbali za kisiasa kupitia

No comments:

Post a Comment