Thursday 14 May 2015

Wananchi 6000 wakosa mawasiliano ya barabara na Umeme baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba Daraja.


Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo kusimama.
Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji  huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa muungano waliopo kata ya goba na  mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo,hali ambayo imewalazimisha kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.

No comments:

Post a Comment