Usafiri wa Treni kuelekea Mwanza na Kigoma umestishwa kwa muda
Kampuni ya reli Tanzania TRL imetangaza kusitisha safari zake za treni
ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma kwa
tarehe 19 na 21 kutokana na matengenezo makubwa ya daraja katika njia
ya treni mkoani Morogoro.
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa TRL Bwana Focus Makoye amesema safari zitaanza
mara baada ya matengenezo hayo tarehe 21 Septemba 2017 na kwamba kati
ya abiria 2000 wataathirika kutokana nakusitishwa kwa safari hizo.
No comments:
Post a Comment