Sunday 24 September 2017

6 wajeruhiwa kwenye shambulizi la tindi kali London

Watu 6 wamejeruhiwa huko Stratford mashariki mwa London kwenye kile kinachotajwa kuwa shambulizi la tindi kali.
Polisi waliitwa kwenda huko Stratford kufuatia makabiliano kati ya makundi mawili ya wanaume ambapo kitu kilirushwa.
Watoa huduma za dharura waliwatibu wanaume sita katika eneo hilo na watatu kati yao wakapelekwa hospitalini.
Kijana wa kiume wa umri wa miaka 15 amekamatwa kwa kushukiwa kusababisha majeraha mabaya ya mwili.
Wale walioripotiwa kujehiwa waliaminiwa kuwa maeneo tofauti hali iliyozua kuwa watu walikuwa wamerushiwa tindi kali hiyo kiholela.
Hata hivyo polisi walisema kuwa wale waliojeruhiwa walikuwa walihusika na shambulizi la awali.
Hakuna mtu aliyepaya majeraha ya kutishia maisha au kubadilisha maisha.
Walioshuhudia wanasema kuwa majibizano yalikuwa yamezuka kati ya kundi la watu.
Mwanamume mmoja ambaye alitajwa jina kama Hossen ambaye ni meneja wa mgahawa mmoja, alisema kwa muathiriwa akikimbia kwenda kwa mgahawa kuasha kuosha tindi kali hiyo kutoka kwa uso wake.

"Alikuwa na majeraha kwenye uso na alikuwa anajaribu kuyamwagia maji," alisema Hossen
.

No comments:

Post a Comment