Wednesday 27 September 2017

Wakurd wasisitiza kujitenga na Iraq

Mmoja wa maofisa waandamizi katika serikali ya Iraq,katika jimbo la Kurd amesema kuwa kwa sasa suala la uhuru wa eneo hilo ni jambo lisilozuilika kutokana na utata wa kura ya maoni.
Falah Mustafa Bakir ambaye ni waziri wa uhusiano wa kimtaifa ameiambia BBC kuna uwezekano uhuru huo ukapatikana ndani ya mwaka mmoja.
Amesema kuwa mazungumzo kati ya serikali ya Iraq hayapaswi kuwa na kikomo, Matokeo rasmi ya kura ya maoni ya siku ya jumatatu haitatangazwa,lakini kiongozi wa Kurdi Massoud Barzani, anasema wapiga kura wamechagua kuwa huru.

Serikali ya Iraq kwa nguvu zote inapinga upigaji kura hizo za maoni na inadai kuwa mamlaka ya Kikurdi inapaswa kusalimisha uwanja wa ndege wa Baghdad ama kuwa tayari kukabiliana na hatua za kimataifa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment