Saturday 30 September 2017

Roketi kuanza kusafirisha watu



Itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Hivi karibuni watu wataweza kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kutumia roketi, safari ambayo itachukua dakika chache tu, kulingana na mjasiriamali Elon Musk.
Musk aliahidi haya katika kongamano moja nchini Australia.
Inasemekana kuwa itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Musk amesema pia kuwa mwaka wa 2024, ataanza kuwasafirisha watu hadi Mars. Kampuni yake ya SpaceX itaanza kujenga meli za kipekee zitakazofanikisha haya, mwaka ujao.
Kwa sasa kampuni yake inatengeneza ain amoja tu ya roketi; aina ya BFR ambayo inaweza kufanya kazi tofauti tofauti ikiwemo kupeleka watu kwenye mwezi na Mars.
"Safari ambazo watu wengi wanaona kuwa ndefu zinaweza kukamilika kwa chini ya nusu-saa," aliambia umati wa watu mjini Adelaide.
"Baadhi ya wateja wetu wanataka kuona BFR ikiruka mara kadhaa kabla yaya kuwa na imani nayo," Musk alisema.
"Kwa hivyo tunachotaka kufanya ni kujenga roketi kadhaa aina ya Falcon 9 na Dragon, ili wateja wawe na urahisi, na ikiwa wanataka kutumia roketi za kale, bado tuna kadhaa."
Musk, alianza mipango ya kufanikisha safari za Mars mwaka wa 2016, na amerejea na habari zaidi.
Musk amevutia watu wengi sana ambao wamependezwa na miradi yake. Na ingawa ahadi zake mara nyingi zimechukua muda mrefu kutekeleza, baadhi imetimia.

Hii ni pamoja na kutuma na kurejesha roketi 16 duniani baada ya roketi hizo kumaliza misheni yao. Roketi mbili kati ya hizo 16 zimeweza kusafiri tena mara ya pili.

Anasema cha muhimu sana kwake ni kuunda rtoiketi ambazo zinawza kutumika tena na tena kama ndege, kwani ni inagharimu pesa nyingi sana kutengeneza roketi.

No comments:

Post a Comment