Wednesday 27 September 2017

Meya aweka mambo hadharani



  Meya wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob ameeleza kuwa kesho atafika katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuzungumzia shauri lake la vyeti dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza  leo Jumatano, Jacob amesema wiki iliyopita amepokea barua kutoka sekretarieti wakimtaarifu kwamba wiki hii ndiyo wanalifanyia kazi shauri lake.
“Wananitaka kwamba baadhi ya mambo niliyoyaongea wananitaka na mimi nipeleke vielelezo vya ufafanuzi lakini kimsingi ni mambo mapya, yaani kana kwamba mtuhumiwa wangu mambo ya vyeti amekiri, amekubali.”
Jacob amesema akitoka kwenye mahojiano hayo na Sekretarieti ya Maadili ataongea na vyombo vya habari juu ya shauri hilo kuhusu kugushi vyeti na malalamiko mengine manne.
Mbali na hilo amesema atazungumzia vishawishi na vitisho katika kulimaliza shauri hilo lisiendelee.

“Kutoridhika na mwenendo wa shauri hilo linavyofanywa kwa kuchelewa na usiri mkubwa sana.”

No comments:

Post a Comment