Friday 29 September 2017

Serikali Yaipongeza Muhimbili kwa Kutoa Huduma Bora

0001A
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya (kulia) akitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo ili kuona maeneo mbalimbali yaliokarabatiwa vikiwamo vyumba vya upasuaji na vyumba vya kulaza wagonjwa wa figo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
0002
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Uzingizi leo pamoja na watumishi wengine wa hospitali hiyo
0003
Baadhi ya wafanyakazi wa idara hiyo pamoja na watumishi wengine mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya  leo.
0004
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo leo.
0005
Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwamo wa Idara ya Usingizi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Museru.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Dar es salaam
Serikali imepongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) za kuboresha huduma  sanjari na kuwawezesha  watalaam kusoma ili wapate ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulusubisya wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.
Dk. Mpoki amesema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na uongozi wa hospitali na kwamba hatua hiyo inaleta faraja kwa Watanzania kwani sasa wana uhakika wa kupata huduma bora .
“Naona mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji, Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha  huduma zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu  mna watalaam wengi waliobobea hapa,’’ amesema Dk. Mpoki.
Kuhusu kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate ujuzi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.
Dk. Mpoki ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dk. Doroth Gwajima pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo vyumba vya upasuaji, wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya watoto.
 

No comments:

Post a Comment