Friday 22 September 2017

Akamatwa kwa kunyoosha kidole cha kati akiwa barabarani

Mwamume mmoja raia wa Uingereza ambaye alinyenyua juu kidole chake cha kati cha mkono wake akimuonyesha dereva mjini Dubai anakabiliwa na uwezekano wa kushtakiwa kwa "tabia ya uhalifu wa maadili".
Jamil Ahmed Mukadam, kutoka eneo la Leicester, amesema kuwa aliamua kufanya hivyo " baada ya kukasirika" pale dereva alipompita barabarani.
Tukio hilo lilitokea mwezi Februari, lakini alikamatwa tarehe 10 Septemba aliporejea Dubai kwa mapumziko mara ya pili.
Pasipoti yake imehodhiwa na Bwana Mukadam ameambiwa kuwa ni lazima abaki jijini dubai asubiri kesi yake.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uingereza amesema kuwa : " Tunajaribu kumsaidia raia wa Uingereza ambaye alikamatwa jijini Dubai na tunaendelea kuwasiliana na mamlaka za mji huo." kumsaidia
Bwana Mukadam, ambaye anafanyia kazi kitengo cha Teknolojia ya mawasiliano ya serikali ya Uingereza, amesema kuwa hakufahamu kuwa alikuwa na kesi ya kujibu aliporejea Dubai.
" Ninahofu ya kuishiwa na pesa hata kabla ya kesi yangu kuanza ,"alisema.
" Hakuna mtu anayepanga kuishi miezi miwili au zaidi hotelini mjini Dubai.
Shirika linalofahamika kama Detained in Dubai linawaonya wageni wanaouzulu mji huo kwamba wanaweza kutiwa nguvuni kwa tabia zifuatazo ambazo huenda ni za kawaida nchini mwao kama vile:
Kulala chumba kimoja na mtu ambaye ni wa jinsia tofauti ambaye hamjaoana
Kushiriki ngono na mtu wa jinsia sawa na yako
Kutembea hadharani ukiwa umeshikana mkono ama kumbusu mtu kwenye shabu hadharani
Kubishana ama kuonyesha dharau kwa mtu mwingine
Kuapa ama kuonyesha ishara za ukatili
Unywaji wa pombe hata katika maeneo yaliyoidhinishwa

Kuvaa mavazi ya kubana mwili kama vile suruari za jinzi

kwa mwanamke kutofunika mikono ama miguu yake

Na matendo ya wapenzi wa jinsia moja

No comments:

Post a Comment