Monday 25 September 2017

Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuanza Mkutano wa saba siku ya Jumatano tarehe 27 Septemba mwaka huu

01
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mkutano wa saba wa Baraza la tisa la Wawakilishi huko Chukwani Zanzibar.
02
Mshauri wa Baraza la Wawakilishi mambo ya sheria Mussa Kombo Bakari akitowa ufafanuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya Waandishi wa habari huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar.

Na  Khadija Khamis –Maelezo  
Katibu wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar Raya Issa Mselem amesema Mkutano wa saba wa Baraza la Wawakilishi unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 27 Septemba mwaka huu .
Aliyasema huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawaklishi  Chukwani nje kidogo ya Zanzibar wakati akizungumza na waandishi  kutoka katika  vyombo mbali mbali vya habari
Alisema shughuli ambazo zinatarajiwa kufanyika katika mkutano huo ni maswali 136 ambayo yanatarajiwa  kujibiwa katika kikao hicho pamoja na miswaada miwili itawasilishwa kwa mara ya pili katika kikao hicho.
Aidha alisema mswada  itayowasilishwa  ni mswada wa sheria yakufuta sheria ya mahakama ya kadhi namba 3 ya 1985 na kuanzishwa upya mahakama ya kadhi na kuweka masharti menghine yanayohusiana na hayo na mswada mengine ni mswada wa sheria yakuanzishwa baraza la taifa la biashara na kuweka mambo mengine yanayohusiana na hayo.
 
Alieleza kuwa katika mkutano huo pia utapokea  ripoti za utekelezaji  wa Wizara  za SMZ  kuhusu maagizo ya kamati za kudumu za baraza pamoja taarifa za seriikali na ripoti za utekelezaji wa mamlaka ya maji Zanzibar(ZAWA).

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment