Thursday 28 September 2017

Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

001
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
002
Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
003
Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
004
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
005
Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionyesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.
006
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru (kaunda suti) akiwa kwenye mkutano huo leo.
007
Mkurugenzi wa hospitali hiyo akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya MNH na wadau mbalimbali.

Dar es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia  kuwahudumia watoto wachanga( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.
Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu  unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa  kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .
‘’ Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka  26 kwa kila vizazi hai 1,000 na kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa hapa   ni takribani  10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta mabadiliko makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.
 
Pia ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto mwenye vimelea vya bakteria.
Akiwasilisha mada kuhusu muongozo  huo , Daktari wa watoto  , Jullieth Cosmas ametaja sababu zinazochangia  watoto wachanga kulazwa Hospitalini  kuwa ni  mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti)  mtoto kushindwa kupumua vizuri pindi anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia wakapi alipozaliwa na mtoto kuumia wakati akizaliwa.

No comments:

Post a Comment