
"Ujasiri ni nini ?
Zitto Kabwe
Nimetumia wikiendi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu jijini Nairobi.
Nimerudi nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwasababu ya nguvu na ujasiri
ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.
Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini
namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi.
Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza.
Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.
Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu
yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana
kama asingesema maneno haya kwangu "tumeshinda.
Tumeshashinda".
Ujasiri ni Lissu"
No comments:
Post a Comment